Jamani nawaulizeni

10

 

Jamani nawaulizeni,
Swali langu mnijibuni,
Ikiwa sote shughulini,
Nadhifu atakuwa nani?

14Pilika na purukushani,
Zikikita humu duniani,
Nayo mambo nyeti kubuni,
Mawazo yatakuwa fani?

Bado nasisita banani,
Mbona banati uhunini,
Waja waaga faraghani,
Na majibu hayawiani?

Adinasi akifa jamani,
Nazidi kuwaza makini,
Hatima yake kweli gani,
Mathalani bila imani?

1Uvumi sina sinani,
Uwongo hata abadani,
Kweli tawafahamisheni,
Nao ni Yesu msalabani.

 

Advertisements

2 comments on “Jamani nawaulizeni

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s